January 3, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BREAKING NEWS: Mbunge afariki ajali ya pikipiki

Na ,Esther Macha, Timesmajira,Online, Mbarali

MBUNGE wa Jimbo la Mbarali , Francis Mtega amefariki dunia baada ya kupata ajali ya pikipiki aliyokuwa akiendesha kugongana uso kwa uso na Powertiler na kupelekea umauti kumfika.

Ajali hiyo imetokea kata ya Ihai wilayani Mbarali mkoani Mbeya ambapo Mbunge huyo alikuwa akiendesha kuelekea shambani kwake ambapo nyuma alipakia mifuko kwa ajili ya kwenda kuvuna mpunga shambani kwake.

Akizungumza na Timesmajira Diwani wa kata ya Kongolo mswiswi ,Elia Bange amesema kuwa baada ya ajali hiyo kutokea majeruhi alikimbizwa hospital ya Chimala na kuwa kabla ya kupatiwa matibabu alifariki katika hospitali ya mission ya ChimalaMwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ,Twalibu Lubandamo amekiri kutokea kwa kifo cha Mbunge Mlwa jimbo hilo Francis Mtega kilichosababishwa na pikipiki aliyokuwa akiendesha wakati akielekea shambani kwake kata ya Ihai .

“Hivi sasa tupo njiani tunaelekea hospitali ya wilaya ya wilaya kwa ajili ya kwenda kuhifadhi mwili wa Mbunge wetu wakati tukisubiri taratibu zingine”amesema Mwenyekiti huyo wa halmashauri.

Mkuu wa wilaya ya Mbarali ,Col.Denis Mwila amekiri kutokea kwa ajali hiyo ambapo anesema tukio hilo limetokea majira ya 15.30 alasiri eneo la kibaoni ambapo marehemu mtega alikuwa akiendesha pikipiki aina ya Boxer yenye namba MC 573 CGT .

Amesema kuwa Powertiler aina ya kubota iliyokuwa ikiendeshwa na Alex Musa (18) mkazi wa kibaoni ilikuwa ikitoka kapunga ilimgonga mwendesha pikipiki huyo ambaye ni mbunge wa Jimbo la Mbarali na kusababisha umauti.

Aidha Col.Mwila amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo uzembe wa opareta wa Powertiler kwa kutochukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara.

Mtuhumiwa wa Powertiler amekakatwa yupo kituo cha polisi Chimala.Hata hivyo marehemu Mtega licha ya kuwa Mbunge pia alikuwa Mwenyekiti wa parokia ya Chosi kata ya Chimala.Mwisho.