Na Mwandishi Wetu
MADAKTARI 610 walioomba nafasi za kazi zilizotangazwa na Serikali kuanzia Machi 24 hadi Aprili 2020 mwaka huu wametakiwa kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa kuanzia Jumatatu Mei 11, hadi Mei 25, mwaka huu.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Ofisi ya Rais-TAMISEMI) zoezi la uchambuzi wa maombi ya kazi ya madaktari yaliyopokelewa limekamilika, hivyo waliokidhi vigezo wamepangiwa kazi katika vituo vya afya na hospitali mbalimbali za Halmashauri nchini.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, madaktari wote waliopangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Serikali.
Maelekezi hayo ni pamoja na kutakiwa kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa katika halmashauri mbalimbali nchini, kuanzia Mei 11, 2020 hadi 25 Mei, 2020.
Taarifa hiyo imesema waombaji watakaoshindwa kuripoti kwenye vituo vya kazi walivyopangiwa kwa tarehe hizo bila ya taarifa, nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine wenye sifa haraka iwezekanavyo.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best