MTWARA, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara,Wakili Msomi Evod Mmanda amefariki dunia alfajiri ya leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara, Ligula.
Duru za habari kutoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikalini ziliudokeza mtandao wa Timesmajira Online kuwa, Wakili Msomi Mmanda kabla ya kifo aliwahi kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili miezi minne iliyopita kwa shinikizo akaruhusiwa.
Aidha, mauti imemkuta akiwa amelazwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula, akisumbuliwa na maradhi ya moyo.
Mmanda aliteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Mtwara na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Jonh Magufuli, Desemba 19, 2016 akichukua nafasi ya Dkt. Khatib Kazungu ambaye alihamishiwa Wizara ya Fedha.
Wakili Msomi Mmanda aliyewahi kuwa pia mjumbe wa Bunge la Katiba. Katika Bunge hilo, aliteuliwa na Mwenyekiti wa muda wa vikao vya Bunge Maalumu la
Katiba, Pandu Ameir Kificho, kama mmoja ya wajumbe 20 watakaomshauri ili kuboresha utendaji.
Kwa habari hii na nyingine nyingi soma Gazeti la Majira
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria