December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Aliyekuwa DAS Handeni, Marehemu Boniface Maiga enzi za uhai wake

BREAKING NEWS: DAS wa Handeni afariki katika ajali mbaya

TANZIA TANZIA

Mnamo saa 7 usku maeneo ya Vikonji Dodoma tumempoteza DAS HANDENI Comred Boniphace Maiga katika ajali ilihusisha gari la Omari Kigoda ambaye ni Mbunge wa Handeni na Bus aina ya Tata.

Gari la Kigoda lilikua na watu wanne akiwemo Omari Kigoda, DAS, Dereva na Msaidiz wa Kigoda.

Hali za wengine zinaendelea vizuri katika Hosptal ya Rufaa ya Dodoma.

Mwili wa Marehemu Bonface Maiga upo Hosptal ya General.

Hakika Maisha yetu ni mafupi mno.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela akiwa na Katibu wa CCM wa Mkoa wa Tanga wakimjulia hali Mbunge wa Handeni Mjini Omari Kigoda alipokuwa anapatiwa Matibabu Hospitali ya Rufaa ya Jijini Dodoma leo usiku wa saa nane baada ya kutoka kwenye eneo la tukio la ajali iliyopoteza maisha ya DAS Handeni Boniface Maiga aliekuwa safari moja na Mbunge .
Gari lilikuwa lilipata ajali na kusababisha kifo cha DAS wa Handeni usiku wa kuamkia leo