Na Mwandishi Maalum, TimesMajira Online
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) makao makuu inamshikilia aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Madawa nchini (MSD), Laurian Bwanakunu.
Hayo yamebainishwa muda huu kupitia taarifa iliyotolewa na Afisa Uhusiano TAKUKURU makao makuu, Doreen Kapwani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, pamoja na Mtendaji Mkuu huyo yupo Kaimu Mkurugenzi wa Logistiki wa MSD, Byekwaso Tabura ambao wote kwa pamoja wapo mahabusu katika ofisi za TAKUKURU Upanga jijini Dar es Salaam kuanzia leo ili kupisha uchunguzi.
Watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma kuhusu matumizi mabaya ya madaraka pamoja na kuisababishia Serikali hasara kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Rais Samia afanya uteuzi