December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BREAKING NEWS: Ajali ya basi yaua, yajeruhi makumi wilayani Karatu

Na Sophia Fundi, TimesMajira Online, Karatu

WATU kadhaa wanaripotiwa kufariki dunia huku zaidi ya 20 wakijeruhiwa katika ajali ya basi iliyotokea eneo la Kilimatembo wilayani Karatu Mkoa wa Arusha.

Ajali hiyo imetokana na basi la Coast Line lenye namba za usajili T.405 AME ambalo lilikuwa likitokea mjini Musoma, Mara kwenda jijini Arusha.

TimesMajira Online ikiwa katika eneo la tukio muda huu imeshuhudia miili ya watu wanne ikitolewa huku majeruhi wakikimbizwa katika Hospitali za Karatu Lutherani na Rotia wilayani humo.

Wasamaria wema wakiendelea kusaidia kuokoa watu muda huu katika eneo la ajali. (Picha zote na Sophia Fundi, TimesMajira Online)

Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo, Abdala Juma ameeieleza TimesMajira Online kuwa, basi hilo lilishindwa kukata kona na kufeli breki, hali iliyosababisha lipinduke, hivyo kuwalalia abiria, ambapo majeruhi walionekana katika hali mbaya huku wengine wakiwa hawajitambui.

Kwa kina fuatilia hapa