Na Grace Gurisha, TimesMajira,Online Dar
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Mkulima, Cosmas Chacha (45), kifungo cha miaka 15 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kuwakeketa watoto wake watatu wa kike wenye umri wa chini ya miaka 18, huku akijua kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria.
Aidha, Chacha (Mkurya) anatakiwa kulipa fidia ya sh. milioni moja kwa kila mtoto kutokana na majeraha aliyowasababishia watoto wake.
Hukumu hiyo, imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa mashtaka, vielelezo vitatu (PF3) pamoja na vifungu vya sheria.
Chaungu amesema upande wa mashtaka wameweza kuthibitisha mashtaka ya ukeketaji huo bila kuacha shaka lolote kama sheria inavyoelekeza.
“Mshtakiwa Chacha amepatikana na hatia katika makosa yote matatu ya ukeketaji, kila kosa atatumikia kifungo cha miaka mitano jela, ambapo adhabu zinakwenda sambamba, kwa hiyo atatumikia kifungo cha miaka mitano tu,” amesema Chaungu.
Katika maelezo ya awali, inadaiwa kuwa mshtakiwa Chacha alikwenda kuwachukua watoto wake hao (majina yamehifadhiwa) katika kituo cha kulelea wa mtoto cha SOS kilichipo Sinza, Dar es Salaam kwa madai kuwa anawapeleka kwa bibi yao Tarime, Mara.
Inadaiwa kuwa mshtakiwa hakuwapeleka watoto wao kama alivyodai na kuwapeleka Kivule, Dar es Salaam sehemu aliyoiandaa kwa ajili ya kuwakeketa watoto wake.
Ilidaiwa kuwa mshtakiwa (Chacha) alitenda kosa hilo Desemba, 8, 2019 maeneo ya Kivule, jijini Dar es Salaam, akiwa baba na mwenye jukumu la kuwatunza watoto hao aliwakeketa na kuwa sababu shida majeraha makubwa.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Rais Samia afanya uteuzi