December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BOT yaanza kununua dhahabu ghafi

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Bombambili, halmashauri ya mji wa Geita.

Kigahe amefahamishwa kuwa pamoja na jitihada zingine katika kuhakikisha nchi inakuwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni, Benki Kuu imeanza kununua dhahabu ghafi kutoka kwa Wachimbaji wakubwa, wadogo na wa kati.

Maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka, yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi Septemba 23, 2023 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko na yatafikia kilele Septemba 30, 2023 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi siku ya kufunga maonesho hayo.

Maonesho hayo yenye kauli mbiu; Matumizi ya teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi mazingira yamewaleta pamoja washiriki zaidi ya 400.