April 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Boshe:ALF imekutana kutambua Maendeleo Endelevu ya Bara la afrika

Na Penina Malundo,Timesmajira

Waziri Mkuu wa Mstaafu wa Ethiopia na Mratibu Mwenza wa Jukwaa la nane la Kikanda la Viongozi Afrika (ALF), Hailemariam Desalegn Boshe amesema wamekutana katika Jukwaa hilo kwa jambo la kutambua maendeleo endelevu ya Bara la afrika.

Ameyasema hayo leo Kampala ,Uganda katika Kongamano la nane la Kikanda la Viongozi Afrika (ALF) lililoanza leo na kumalizia Aprili 8 mwaka huu lililoandaliwa na Taasisi ya Uongozi.

Amesema miongoni mwa mpango wa SDGs kipengele cha 17 kinawakilisha mpango bora wa maisha yajayo na hamu ya pamoja ya kuondokana na umaskini,kutokuwa na usawa na uharibifu wa mazingira.

“Ni wakati wa kutumia teknolojia za kidijitali na kukuza uvumbuzi kunaweza kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha utoaji wa huduma,” amesema.