January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bonnah amlilia mwenezi Makala atatue kilio cha wakazi wa Kipunguni

Na Heri Shaaban,Timesmajira Online,Ilala

MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli ,amewasilisha malalamiko yake kuhusiana na changamoto ya muda mrefu ya wakazi wa Kipunguni kushindwa kulipwa fidia ya maeneo yao kupisha upanuzi wa Uwanja Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.

Bonnah amrwasilisha changamoto hiyo kwa Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Amos Makala, katika mkutano wa hadara baada ya ziara kutembelea Jimbo la Segerea kuangalia uhai wa chama na kuzungumza na wanachama na kupokea kero za wananchi.

“Mwenezi wa CCM Taifa tupelekee salamu kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Samia Suluhu Hassan mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji( DMDP) ufanyike haraka barabara ziweze kujengwa changamoto za Jimbo la Segerea kwanza ni ya kulipwa fidia wananchi wa Kipawa mtaa wa Kipunguni ni changamoto ya muda mrefu zaidi ya miaka 27 Mawaziri wengi wamefika utatuzi wake umegonga mwamba,”ameeleza na kuongeza kuwa;

“Amos Makala tunaomba suala hili unalifahamu wakati ukiwa Mkuu wa Mkoa sasa tunaomba lifike hatua za mwisho baada ya Waziri wa Fedha Mwigulu Mchemba kufika mwaka 2023 alitoa maelekezo Wananchi watalipwa Agosti 2023 nyumba zimevunjwa na hakuna malipo yoyote mpaka sasa 2024,”.

Pia amesema kuwa wananchi wa Kipunguni kwa sasa wanaishi katika Mahema wameshindwa kuliendeleza eneo hilo na hakuna kiongozi yoyote wa Serikali anafika katika eneo hilo.

Akizungumzia mafanikio sekta ya afya Jimbo la Segerea ameeleza kuwa serikali imejenga kituo cha afya Kinyerezi, Segerea,Kiwalani,Plani kilichopo Mnyamani na shule nyingi za sekondari na msingi.

Mwenezi wa CCM Taifa Amos Makala, akijibu changamoto hizo ambapo madai ya Kipawa Kipunguni alimunganisha Waziri wa Fedha Mwigulu Mchemba akaeleza” ni kweli anafahamu changamoto ya Kipunguni yeye Mwenyewe amefika na Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli kufatilia.

“Wizara ya Fedha ni kweli imechelewa kuwalipa wananchi wa Kipunguni na hivi Karibuni itawalipa ilikuwa ,changamoto pia leo (Jana Julai 08 /2024 amekutana na wajumbe wa Kipunguni amezungumza nao baada mwaka wa fedha Agosti 2024 malipo ya Kipunguni yatafanyika,”amesema Mwigulu.

Makala amesema Mbunge amefuatilia miaka yote lakini ameomba radhi wananchi wa Kipunguni kufuatia nchi yetu kupata changamoto za mafuriko hivyo Julai wanaweka mifumo sawa wataanza kulipwa .