December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bonnah aibua shangwe kwa wakazi wa Tabata

Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Ilala

MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonah Kamoli, amewatangazia wakazi wa Jimbo hilo ambao kwa miaka takribani sita wamekuwa wakisubiri kulipwa fidia ili kupisha ujenzi wa barabara ya Mwendokasi awamu ya sita, waendelee kuishi kama kawaida, mpaka Serikali itakapotangaza upya kulipa fidia.

Mmoja wa wakazi wa mtaa wa Mtambani, Paul Abel, alipohojiwa sababu za kushangilia kauli hiyo, amesema kwa miaka sita ameishi bila kukarabati nyumba kwa namna yoyote, wapangaji wamemkimbia hivyo kuathiri hali yake kiuchumi lakini sasa kwa kauli ya Mbunge, ana uhakika wa kurejesha uhai kwa makazi yake.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Tabata Mbunge Bonnah Kamoli ,wakati akieleza utekelezaji wa Ilani na mikakati ya serikali kwa wananchi wa Kata hiyo ameeleza kuwa wakazi wa maeneo hayo waendeleze maeneo yao mpaka hapo Serikali itakapotangaza tena.

Pia amesema Waziri wa Maji alifika jimboni humo kutatua kero za maji na kubadilisha Watendaji wa DAWASA hivyo maji yatafika maeneo yote.

Akizungumzia kero za Tabata Kisiwani amesema changamoto mtaa huo ni mkubwa lakini hauna shule ya msingi.