Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Mbeya
SERIKALI mkoani Mbeya imesema watanzania walio wengi wanafahamu kuhusu uwekezaji wa maeneo ya asili kwa kilimo na ufugaji huku kukiwa na changamoto kubwa ya mwamko mdogo wa kuwekeza katika hisa na masoko.
Kauli hiyo imetolewa Juni 27,mwaka huu na Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mbeya Donald Bombo wakati akifungua mafunzo yaliyohusisha wamiliki wa kampuni ndogo na kati,wafanyabishara yaliyoratibiwa na Mamlaka ya Masoko ,Mitaji na Dhamana (CMSA ) na kufanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
“Kama Mkoa kupitia mafunzo haya kwa wafanyabiashara wadogo na kati ni watajifunza na kujua umuhimu wa kuwekeza kwenye hisa na masoko kwani asilimia zaidi 90 haitambui umuhimu wa mfumo huo na manufaa yake ”amesema.
Bombo amesema kwa sasa wafanyabiashara walio wengi bado wanajifunza kuwekeza kwenye biashara na kwamba asilimia inayowekezwa kwenye biashara bado ni ndogo haijafikia asilimia 20 na kuwa chini ya asilimia 20.
“Lakini asilimia 80 bado tunawekeza kwenye kilimo na mifugo hivyo tuwakaribishe kuja kuelimisha masoko na mitaji kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa kwenye masuala ya uwekezaji ambapo wengi bado hamfahamu na ukiuliza uwekezaji ni nini bado wengi wetu hatuelewi”amesema Katibu tawala huyo msaidizi.
Mkurugenzi wa Sera,Utafiti na Mipango kutoka Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana ,Jijini Dar es Salaam Afred Mkombo amesema kuwa lengo la semina hiyo ya siku moja kwa wafanyabiashara hao ni kuhusu utaratibu wa biashara kwa kutoa mawazo yao.
Mkombo amesema kuwa changamoto ambayo wameona katika masoko ya mitaji kwenye soko la hisa katika kusaidia biashara kubwa kwenye makampuni makubwa katika kupata mitaji.
“Kuna sehemu ya biashara ndogo na kati zinashindwa kufikia masoko ya mitaji kwa viwango vilivyowekwa kwenye soko la kimataifa”amesema Mkurugenzi huyo.
More Stories
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto
Kilo 673.2,dawa za kulevya zakamatwa Bahari ya Hindi