Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
BODI ya Wadhamini ya TANAPA, Aprili 07, 2025, imeagiza kukamilishwa kwa haraka miradi ya miundombinu ya utalii inayotekelezwa katika Hifadhi ya Taifa Mikumi ili kuvutia watalii zaidi.
Akiwa katika ziara ya ukaguzi, Mwenyekiti wa Bodi, Jenerali (Mstaafu) George Waitara, alisisitiza umuhimu wa kasi na ubora katika utekelezaji wa miradi hiyo.
“Tumejionea uboreshaji unaofanywa hapa Mikumi. Ni dhahiri sasa Mikumi itaongoza katika utalii wa ndani,” amesema Jenerali (Mstaafu) Waitara.

Naye CPA Khadija Ramadhani, Mjumbe wa Bodi na Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi na Utawala Bora, aliishukuru Serikali kwa uwekezaji mkubwa na kuhimiza maandalizi bora ya kuwahudumia watalii.
Naibu Kamishna Massana Mwishawa amesema mradi wa SGR umeongeza watalii na mapato Mikumi, na Shirika linapanga kufungua lango jipya Chamgore karibu na kituo cha Kilosa.
Kamishna Msaidizi Augustine Massesa ameeleza kuwa miundombinu mipya, ikiwemo uwanja wa ndege unaokamilika, imeongeza idadi ya ndege na wageni, na kusaidia kukuza uchumi wa jamii zinazozunguka hifadhi.
Kupitia mradi wa REGROW, Serikali imeendelea kujenga nyumba za kulala wageni (cottages), vituo vya taarifa, maeneo ya kupumzikia na kuboresha uwanja wa ndege Kikoboga.




More Stories
Polisi kuchunguza madai ya mwanafunzi kutupa kichanga chooni
Sekiboko ahimiza uwekezaji Elimu ya ufundi
Wazee wawili jela maisha kwa kubaka na kulawiti