January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bodi ya Utalii yawapokea mawakala 65 kutoka Marekani

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

Kundi la mawakala wa utalii 65 kutoka Marekani wamewasili hapa nchini ili kujifunza na kuutangaza utalii ambao unapatikana hapa nchini

Akizungumza jijini Arusha mapema Jana mara baada ya kuwapokea mawakala hao afisa utalii kutoka Katika bodi ya utalii Tanzania (TTB) Ester Solomoni alisema kuwa ujio huo ni fursa kubwa

Bi Ester alisema kuwa mawakala hao ni fursa kubwa kwa kuwa mawakala hao ndio wanaogawa vifurushi kwa wageni

Aliendelea kwa kusema kuwa ujio huo pia ni matokeo ya uzinduzi wa filamu iliyozinduliwa na Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia suluhu Hasani

“Sisi kama wadau wa utalii Kwa kweli tumefurai sana kuwapokea mawakala hao kama mnavyojua hawa ndio wanaotoa vifurushi Sasa wakiona na kushuhudia utalii uliopi hapa wataweza kuwa mabalozi wazuri hata Kwa nchi Yao ya Marekani”aliongeza

Naye mwenyekiti mstaafu wa bodi ya utalii Tanzania jaji Thomas mihayo alisema kuwa mawakala hao watakachojifunza hapa nchini wataweza kukupelekea Marekani na hivyoo kuwezesha fursa nyingi kuendelea kuwepo hapa Tanzania

Naye Michael makombe kutoka katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro alisema kuwa ujio wa mawakala hao ni matokeo mazuri ya filamu ya Royal Tour na watakapofika katika vivutio basi wataweza kushuhudia uzuri wa vivutio vilivyopo Tanzania.