Na Esther Macha,Timesmajira Online, Mbeya
BODI ya nafaka na mazao Mchanganyiko(CPB) imesema itaingia mikataba na wakuma wa mazao Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kufuatia kuwepo kwa mtandao wa masoko ya uhakika nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mkuu bodi ya nafaka (CPB) Dkt. Anselm Moshi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya 29 ya Sikukuu ya Wakulima (nanenane ) yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya .
Aidha Dkt Moshi alisema kuwa wamekuwa na utaratibu wa kukusanya mazao ya wakulima kuyachakata na kuyaongezea thamani kupitia uwekezaki wa viwanda nane vya kuchakata mazao.
Akielezea zaidi Mkurugenzi huyo amesema kuwa njia ya pili ni mkulima kutumia mtandao mpana wa bodi ya nafaka Tanzania ambao upo ndani na nje ya nchi ambao upo, Congo, Comoro, Kenya, Uganda, Rwanda, Zimbabwe.
“Kwa hiyo tumeanza kujenga mtandao mkubwa wa kuuza mazao ya wakulima na tunaendelea kujenga huo uwezo wa kimtandao ili wakulima wa Tanzania wa alisema mazao ili bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko iweze kununua na kuhifadhi kwenye miundo mbinu yake” amesema Mkurugenzi huyo.
Hata hivyo Dkt.Moshi amesema wanataka wakulima wafahamu kuwa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko ina bidhaa bora ambazo zimeandaliwa kwa umakini mkubwa Kwa kutumia watalaam wa bodi hiyo.
John Mwakinywa ni mkulima wa zao la Alizeti katika wilaya ya Mbeya Vijijini amesema kuwa uwepo wa bodi hiyo utakuwa msaada mkubwa Kwa wakulima.
“Tunaamini kuwa sisi tutapata Neema sasa na tutaweza kulima mazao yetu sasa kwa tija hii bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko ni Neema kwetu sasa tujikite kuzalisha kwa ubora” Amesema mkulima huyo.
Mkulima mwingine Peter Juma amesema kwamba kilimo kinatakiwa kiwe mkombozi kwa mkulima hivyo uwepo wa bodi hii utaweza kuwainua wakulima waliokata tamaa ya kilimo. Mwisho.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best