November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bodi ya kahawa Tanzania kuendelea kuzalisha miche bora ya kisasa

Na Esther Macha, Timesmajira Online,Songwe

BODI ya kahawa Tanzania imesema kuwa imeweka mkakati wa kuhakikisha wanaongeza uzalishaji kutoka miche milioni 13 mpaka miche 20 milioni ifikapo mwaka 2025 kwa lengo la kuwezesha wakulima kuongeza tija ya zao hilo nchini kulingana na mahitaji

Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Mkurugenzi mkuu bodi ya kahawa Tanzania,Moses Simwinga wakati wa maadhmisho ya siku ya Kahawa duniani iliyofanyika katika viwanya vya kiwanda cha kukoboa Kahawa Mbozi(MCCCO).

Simwinga amesema katika kipindi hichi ambacho mvua watakuwa wamefikia malengo sambamba na kuhakikisha miche yote inakwenda shambani kwani kumekuwa na changamoto watu wanachukua miche hawapandi shambani .

“Tayari tumewasiliana na vyama vya ushirika kuhakikisha kila mche unaochukuliwa unaenda shambani ,kwa upande wa Kanda ya Mbozi kuna jua kali ingawa tayari serikali imechekua hatua ya kununua gari maalum kwa ajili ya kuchimba mabwawa pamoja na kuwashawishi wadau kuwekeza katika suala la umwagiliaji kama tukimwagilia hata hizi changamoto tulizosikia hazitakuwepo za kiwanda kupata Kahawa chache zisiwepo”amesema.

Aidha Simwinga ameeleza kuwa wakulima wanaendelea kuwekeza kwenye mbegu na miche ili kuhakikisha wanapata miche ya kutosha na wanapeleka nguvu kwenye zoezi la umwagiliaji wakiamiani kwamba kilimo cha umwagiliaji kitachoche kufikisha uzalishaji wa kilo nne na kuendelea lakini kwasasa bado wapo chini.

“Tukiweza kuongeza uzalishaji kwa mtu kwa njia ya umwagiliaji na utumiaji wa mbolea sahihi tutaweza kuhakikisha kuwa hili zao la kahawa ambalo ni uti wa mgongo linatukomboa sisi sote kahawa ni mali inatakiwa tuitunze ili tutimize malengo katika hili mh mgeni rasmi tunaomba utusaidie kurekebisha kutengeneza maeneo ya umwagiliaji,uchimbaji wa visima usafishaji wa mabwawa katika maeneo ambayo tayari kuna mabwawa na kwamba bodi ya kahawa ipo tayari kusaidia zoezi hili ili liweze kufanikiwa “amesema Simwinga.

Mgeni rasmi katika maadhmisho hayo Kaimu mkuu wa mkoa wa Songwe,John Mwaijulu amesema kuwa katika msimu wa mwaka 2023/2024 bodi ya kahawa mpaka imeweza ina jumla ya minada mitatu ya Kahawa ambapo kilo 1,455,501 za kahawa safi zimeuzwa ambazo zimeingiza dola za marekani (USD) ambayo ni sawa na 3,492,718 sawa na Bilion .8,906,430,900.

Mwaijulu amesema biashara ya kahawa ina kipato kikubwa ambapo amewataka kuchangamkia fursa zilizopo katika biashara hiyo na kuwataka wakulima wa kahawa ili waweze kupata bei nzuri iliyoimarika ni vema kuzingatia masharti ya kuandaa kahawa bora.

Akielezea zaidi Kaimu mkuu wa mkoa Songwe amesema kuwa solo la ndani la kahawa ambalo ndilo mkombozi namba moja bado kuna tatizo la kuyumba kwa bei na kuongeza ajira na bado linakuja kwa kasi ndogo na kwamba jambo hilo limeandaliwa kuifanya nchi kutegemea zaidi asilimia 90 ya uzalishaji kwa soko la nje.

“Wito wangu kwa wadau muendelee kuhamasisha kuhusu faida zitokanazo na unywaji wa kahawa na kuondoa dhana potofu iliyojengeka miongoni mwa jamii kuwa kinywaji hiki kina madhara kwa afya jambo ambalo si sahihi na kinyume chake nu kuwa kina faida kubwa kiafya ikiwemo kupunguza magonjwa mbalimbali”amesema.

Mmoja wa wakulima wa Kahawa mkoani Songwe , George Nzunda, amesema kuwa wakulima wa kahawa wamekuwa wakizingatia kilimo kinachotunza mazingira ili kuwa endelevu.