Na Mwandishi Wetu, Times Majira Online
NAHODHA wa klabu ya Simba John Bocco, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Juni katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2019/20.
Bocco ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake Atupele Green wa Biashara United na Martin Kiggi wa Alliance FC alioingia nao fainali.
Hata hivyo, Bocco ametwaa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao 3 kwenye michezo aliyocheza mwezi juni na kuisaidia klabu ya Simba kutwaa ubingwa ikiwa na mechi kadhaa mkononi.
Naye kocha wa Alliance ya Mwanza Kessy Mziray, amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Juni wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2019/2020.
Mziray alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake Sven Vandenbroeck wa Simba na Luc Eymael wa Young Africans alioingia nao fainali.
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM