Na Moses Ng’wat,Timesmajiraonline,Mbozi.
NAIBU Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi,amesema kuwa serikali inatekeleza miradi nane yenye thamani ya sh. Bilioni 13.3 kwa ajili kutoa huduma ya maji katika Wilaya ya Mbozi, Mkoani Songwe.
Mhandisi Mahundi ameeleza hayo leo Novemba 24, 2023, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Wilayani Mbozi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku tatu Mkoani Songwe.
Amesema kuwa jumla ya vijiji 99 vimepatiwa huduma ya maji kati ya Vijiji 121 vilivyopo wilayani Mbozi.
Ameogeza kwa kusema kuwa serikali inaendelea na jitihada za kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji katika miji ya Vwawa na Mlowo wilayani mbozi kupitia mradi wa ukarabati wa chanzo cha maji Mwansyaniawenye thamani ya sh. bilioni 3.9.
Aidha, Mhandisi Mahundi amesema mbali na jitihada hizo, serikali ipo kwenye mchakato wa utekelezaji wa mradi wa maji kwa kutumia chanzo cha maji cha mto Momba ambao unagharimu kiasi cha sh. bilioni 340 kwa ajili ya kutatua kero ya maji katika miji ya Tunduma, wilayani Momba pamoja na miji ya Vwawa na Mlowo, wilayani Mbozi.
More Stories
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake