Na Joyce Kasiki,Timesmajira online. Ruangwa
ZAIDI ya shilingi bilioni zimetumika katika mwaka wa fedha 2021/2022 katika ujenzi wa barabara zinazoelekea katika maeneo migodi Wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya madini yanayoendelea wilayani humo,Meneja wa Wakala wa Barabara za mjini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Ruangwa Mashaka Narubi amesema kuwa pia katika mwaka huo wa fedha wamejenga barabara za lami maeneo ya mji wa Ruangwa ambazo zinaelekea maeneo yote ya migodi ambapo zimegharimu shilingi bilioni 5.2.
Amesema lengo la ujenzi wa barabara hizo ni kurahisisha shughuli za uchimbaji wa madini Wilayani humo ili ziweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka.
“Kwenye mpango wetu wa mwaka 2021 mpaka mwaka 2023 tumejengaa jumla ya madaraja madogo 47 ambapo shilingi bilion 1.5 zilitumika katika ujenzi huo na nadaraja yotectuliyoyajenga maeneo ya vijijini ambapo kama fusa kwa wachimbaji wetu wa madini”amesema mashaka.
“Mwaka huu wa fedha 2023/2024 tunakusudia kujenga barabara kilomita 110 kuelekea maeneo ya madini ambapo tunatarajia kutumia bilion 3.4 kwa ajili ya barabara katika maeneo ya madini”ameongeza.
Pia amesema Tarura Wilaya ya Ruangwa imejilita zaidi kuboresha barabara zinazoelekea kwenye maeneo yenye fursa ya madini ambapo wanaamini kwakufanya hivyo wawekezaji wa madini wajitokeza kwa wingi wilayani humo.
Mashaka ameongeza kuwa mbali na kujenga barabara hizo pia wana mpango wakuongeza barabara nne ambazo ziraelekea kw4nye maeneo kwenye maeneo ya madini kwa kiwango cha lami kutoka Ruangwa kuelekea eneo la Nangurugai ambapo kuna mgodi wa madini ya Graphite ambapo amesema wameshaanza usanifu na mwezi wa kumi mwaka huu wataanza ujenzi wake ambao itakuwa kilometa 31.
More Stories
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme