Na Sophia Fundi, Timesmajira Online,Karatu
Halmashauri ya Wilaya ya Karatu mkoani Arusha kupitia Wakala wa Maji Safi na usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa )imepokea zaidi ya bilioni 1 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa PforR unaolenga kuboresha sekta ya maji ,afya na elimu.
Akizungumza katika uzinduzi wa utekelezaji wa mradi huo Meneja Ruwasa Wilaya ya Karatu Mhandisi Magai Kakuru amesema kuwa mradi huo unatekelezwa katika idara tatu ambayo ni idara ya maji,afya na elimu huku Msimamizi Mkuu akiwa idara ya maji.
Magai amesema kuwa lengo la mradi ni kuboresha huduma katika idara hizo ambapo kwa upande wa idara ya afya ni pamoja na usafi wa mazingira bora kwa kujenga vyoo bora katika taasisi zilizoko vijijini na kaya moja moja.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu John Lucian amewataka Madiwani kushirikiana katika kutekeleza mradi huo kwa kata zote zilizopata ili ukamilike kwa muda uliopangwa.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu Lameck Karanga kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo
Dadi Kolimba amewataka watalaam ,madiwani na watendaji kusimamia utekelezaji wa mradi huo kwa wakati kwani muda uliotolewa ni mdogo na kuhakikisha Wilaya inanufaika.
“Ikumbwe kuwa mradi wa PforR unatekelezwa chini ya Wizara tatu maji , elimu na afya hivyo kila idara isimamie ipasavyo eneo lake ili Wilaya ijizolee fedha zake kwani hii ni kama mbegu unayootesha shambani utegemee kuvuna,”amesema Karanga.
More Stories
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto
Kilo 673.2,dawa za kulevya zakamatwa Bahari ya Hindi