Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
BENKI ya NMB imeanzisha dirisha maalumu la kuwahudumia Watanzania wanaoishi nje ya nchi, huduma ambayo
serikali imesema itasaidia kuongeza fedha
wanazotuma diaspora na kuwekeza nchini.
Suluhisho hilo linaloitwa NMB Kwetu
limezinduliwa rasmi mwishoni wiki iliyopita ili kutoa huduma za kifedha kwa diaspora kwa kuwapa nafasi ya kufungua akaunti na kufanya miamala kidijitali pamoja na kuweza kuwekeza nyumbani kupitia benki hiyo.
Mgenirasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stephen
Mbundi, aliyemwakilisha waziri January
Makamba.
Kiongozi huyo amesema mbali na huduma
hiyo kurahisisha utumaji wa fedha pia
itaongeza fedha hizo za kigeni wanazotuma wana diaspora nyumbani.
“NMB Kwetu ni huduma muhimu
inayoenda kusaidia juhudi za serikali za
kuhakikisha Watanzania wote popote
walipo wanapata huduma za kifedha,
wakiwemo wale wanaoishi ughaibuni,”
Balozi Mbundi amebainisha.
Aidha, ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita inatambua na kuthamini mchango wa diaspora katika ujenzi wa taifa kupitia utaalamu wao na fedha wanazotuma nyumbani ambazo zilifikia dola za Kimarekani milioni 369.3 mwaka 2021.
Balozi Mbundi amesema kiasi hicho
kimekuwa kinaongezeka mwaka hadi
mwaka na kufikia dola bilioni 1.1 sawa na
sh trilioni 2.6 mwaka jana ambapo diaspora walitumia sh bilioni 4.4 kuwekeza katika ununuzi wa nyumba na viwanja nchini.
Amesema kuwa Watanzania hao pia ni washiriki wazuri katika soko la mitaji na
hisa ambapo mwaka 2022 waliwekeza sh
bilioni 2.3 kwenye Mfuko wa Dhamana ya
Uwekezaji (UTT).
“Bila shaka diaspora wetu watachangamkia na hatifungani ya NMB
Jamii Bond ambayo sasa hivi iko sokoni,”
Balozi Mbundi alibainisha huku akitambua
mchango wa Benki ya NMB katika shughuli za maendeleo.
Amesema mbali na kuwa jambo la kihistoria, huduma ya NMB Kwetu pia imekuja wakati muafaka na inatoa fursa kwa benki hiyo kunufaika na miamala ya kimataifa.
Balozi Mbundi ameongeza kuwa kipengele
cha bima ya maisha cha suluhisho hilo
kitatua changamoto ya muda mrefu ya wana diaspora pindi walipokuwa wakikabiliwa na madhira ya vifo au ulemavu wa kudumu.
Afisa Mtendaji Mkuu Benki ya NMB,
Ruth Zaipuna amesema mbali na fao la kifo na ulemavu, bima hiyo pia inagharamia usafirishaji wa maiti huku akitaja sifa kubwa ya kwanza ya NMB Kwetu kuwa ni kutengeneza mfumo wa kidijitali wa ukusanyaji wa nyaraka zinazohitajika kwa ajili ya kufungua akaunti.
“Suluhisho la pili kupitia NMB Kwetu,
ni bima ya maisha. Wana diaspora wote
watakaofungua akaunti zao Benki ya NMB
moja kwa moja watakuwa wameingia bima ya maisha yenye thamani ya hadi TZS milioni 29.”
“Bima hii ya maisha inatolewa kwa
ushirikiano na Kampuni ya Bima ya Sanlam Life.”
“Akaunti zote za NMB Kwetu hazitakuwa
na makato ya kila mwezi kama akaunti
nyingine,” Zaipuna alifafanua na kusema
utumaji wa fedha utaongezewa ufanisi na
huduma ya Worldwide Pesa.
“NMB ilianzisha huduma hii inayowezesha
wana diaspora kutuma pesa nyumbani
kwa ndugu, jamaa na marafiki kutoka
nchi zaidi ya 100 duniani mwaka jana kwa
kushirikiana na kampuni za Thunes na
Terrapay.”
Pamoja na kutotangazwa, Zaipuna
amesema mpaka sasa Worldwide Pesa tayari imefanikisha zaidi ya miamala 35,000 yenye thamani ya zaidi ya sh bilioni 52.
“Fursa za uwekezaji kwa wenzetu
waliopo diaspora pia ni kipaumbele chetu.
kupitia NMB Kwetu, wateja wetu, wana
diaspora watapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba, fursa za kuwekeza kwenye amana za muda mfupi na na amana za muda mrefu zenye viwango shindani na na nyingi pia zikiwa na bima ya maisha,”
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi