Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Leo Benki ya NMB imeaandika historia!
Wametoa gawio la Tsh. Bilioni 45.5, ikiwa ni gawio kubwa zaidi kuwahi kutolewa na Taasisi ya kifedha kwa Serikali. Gawio hili kwa serikali ni kiashiria tosha cha Azma yetu ya kuhakikisha tunaleta tija na faida kubwa kwa wawekezaji wetu wote, ikiwemo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi – Dkt. Edwin Mhede pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu – Ruth Zaipuna, wamemkabidhi Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Dkt Samia Suluhu Hassan mfano wa hundi ya gawio hilo katika sherehe ya maadhimisho ya mikaa 25 ya mafanikio ya Benki ya NMB, inayoendela katika ukumbi wa Mlimani City – Dar es Salaam. Wakishuhudia ni Waziri wa Fedha na Mipango – Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, Msajili Wa Hazina Ndg Nehemia Mchechu, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania – Ndg. Emmanuel Tutuba pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
More Stories
Serikali yahimiza wananchi kutembelea vivutio vya utalii
Magunia ya kufungia tumbaku yakamatwa
Madereva 16,Mwanza wafungiwa leseni ya udereva