Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Benki ya NMB imeendelea kuunga mkono juhudi ya Serikali kupitia Wizara ya Sayansi, Elimu na Teknolojia, kwa kudhamini na kushiriki Wiki ya Ubunifu Tanzania 2023 yenye kauli mbiu ya ‘Ubunifu kwa Uchumi Shindani’ inayofanyika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.
Ushiriki huo una lengo la kuwawezesha wabunifu kujionea na kujifunza bunifu za kiteknolojia za masuluhisho ya kifedha, na kuweza kujaribu masuluhisho yao kupitia mfumo wa ‘NMB Sandbox environment’ ambayo inatoa fursa kwa wabunifu wa masuala ya kifedha kuweza kufanya majaribio ya bunifu zao na kisha kuwasaidia wabunifu hao kuingia sokoni.
Benki hiyo imetenga kiasi cha Bilioni moja kwa ajili ya kuwasaidia wabunifu wanaochipukia kuweza kuziweka bunifu zao katika utekelezaji ili waweze kunufaika, lakini kiasi hicho sio mkopo bali ni fedha iliyotengwa kwa dhumuni ya kusaidia wabunifu hao na hawatawajibika kuirejesha.
Benki hiyo ipo kwenye viwanja vya Jamhuri – Dodoma wiki nzima. Tembelea banda lao kujua zaidi kuhusu suluhishi za kidijitali.


More Stories
Exim yatangaza mafanikio makubwa na mwelekeo madhubuti 2025
Benki ya Exim yakabidhi madarasa kwa shule mbili za sekondari Kigoma
Mwenendo Soko la Hisa, wengi wavutiwa kuwekeza katika Bondi