Benki ya NMB Tanzania na Klabu ya Yanga zimezindua Kadi Maalum za Wanachama wa Yanga, ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano kati ya taasisi hizi mbili kubwa nchini.
Kadi hii ya NMB Yanga World Debit Mastercard imeunganishwa na akaunti na huduma zote za kifedha za Benki ya NMB.
Faida za Kadi hii ni pamoja na:
➡️ Jezi 6 Kila Msimu, VIP Ticket 10 za Msimu
➡️ Kutumia VIP Lounge katika viwanja vya ndege vya kimataifa bure.
➡️ Bima za safari ukilipia tiketi ya ndege kutumia kadi hii ikiwemo kulipwa hadi Dola za Kimarekani 3,000 begi likipotea, hadi Dola 300 ndege ikichelewa na kupata mpaka Dola 7,500 kama safari yako ya ndege ikihahirishwa.
➡️ Punguzo la kuanzia 10% na kuendelea ukitibiwa katika hospitali zote za Aga Khan nchini.
➡️ Punguzo la hadi 10% ukifanya malipo kwa Kadi/QR katika maduka, migahawa, vituo vya mafuta na maeneo mengine.
➡️ Meneja Mahusiano Maalum atakae muhudumia mteja na kumfata alipo kumkabidhi bidhaa atakazonunua kutoka Yanga.
➡️ Mwanachama kupata Toleo la kwanza la jezi na vifaa vyote vinavyotambulishwa na Yanga
➡️ Huduma zote za kifedha zinazotolewa na Benki ya NMB ikiwemo mikopo nafuu, huduma ya NMB Mkononi na nyingine nyingi.
➡️ Mwanachama wa Yanga ataipata kadi hii kwa ada ya Milioni Moja kwa mwaka na kufurahia huduma zote hizi kwa mwaka.
➡️ Kadi hii inapatikana katika matawi yote ya Benki ya NMB nchi nzima kuanzia leo.
Uzinduzi wa Kadi hii umefanyika Makao Makuu ya Benki ya NMB na Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi leo.
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano