January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Benki ya NMB yakutana na viongozi Ofisi ya Waziri Mkuu

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Ujumbe kutoka Benki ya NMB ukiongozwa na Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa Serikali na Ofisi ya Makao Makuu Ndogo ya Dodoma, Bi. Vicky Bishubo kwa nyakati tofauti umemtembelea Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Uratibu na Bunge, Dkt. Jim Yonazi pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Anderson Mutatembwa na kufanya mazungumzo ambayo yanalenga kuimarisha uhusiano kati ya Benki ya NMB na Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Uratibu na Bunge.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Waziri Mkuu – Sera, Uratibu na Bunge zilizopo Jijini Dodoma.