December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Benki ya KCB yatoa msaada kituo cha Maunga Orphanage Center

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Benki ya KCB imetoa msaada wa Vyakula katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Orphanage Center chenye watoto Zaidi ya 30.

Vyakula hivyo
ikiwemo Michele, maharage, mafuta ya kula, tambi, sukari, chumvi na unga wa ngano vina thamani ya shilingi 2,352 000.

Hayo aliyasema Mkuu wa Mahusiano wa Benki hiyo, Christina Manyenye wakati akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.

“Benki yetu inatambua umuhimu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wa kufanya mema na kwakutambua umuhimu huo,tumeamua kurudisha kuja kuwasaidia msaada wa Vyakula mbalimbali kwa kituo hiki cha kulea watoto yatima”Alisema Manyenye.

“Tukiwa kama benki tumekaa kwenye upande angalau mungu ametujalia na wale walioko kwenye jamii ambao wanapata shida na uhitaji KCB Bank tumeliona hilo, tunaliona kwa watoto yatima na tunajua kabisa malezi ya watoto ni magumu sana hasa ninapokua ni mtu mmoja au wawili au kituo kama hivi kulea watoto ambao wapo zaidi ya 30 ambapo wengi ni wadogo sana”.

Pia Manyenye, alisema mbali na msaada huo benki ya KCB imeendelea kuwasaidia makundi mbalimbali ikiwemo kutoa mafunzo ya ujuzi kwa vijana kupitia veta ili waweze kujiajiri na kuwasaidia watanzania wengine.

“Tunaangalia upande wa wanawake pia kujikimu kuwafundisha waweze kuendesha biashara ambazo ni endelevu ambapo uzao wake utakuja kufaidika na kupelekea kupunguza watoto wa mitaani”

Kwa upande Mkuu wa huduma za Benki za kiislamu, KCB Sahl Banking, Amour Muro,alisema benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa watanzania ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Naye,Mkuu wa kituo cha Kulea watoto Yatima cha Maunga Centre,Rashid Matimba,ameishukuru Benki ya KCB kwa msaada huo na kusema msaada huo umekuja wakati muafaka.

“Tunaipongeza benk KCB kwa msaada wao,tunaomba benki zingine waige mfano wa benki hii”Amesema Matimba.