January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Benki ya –KCB yatia saini mkataba wa makubaliano –MOU na Benki ya uwekezaji ya umoja wa Ulaya –EU

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Benki ya –KCB imetia saini mkataba wa makubaliano –MOU na Benki ya uwekezaji ya umoja wa Ulaya –EU, wa mkopo wenye thamani ya shilingi bilioni 50 kwa lengo la kuwawezesha wajasiriamali wanawake Nchini.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo, Mkurugenzi wa –KCB, Cosmas Kimario amesema mkataba huo umechangiwa na mazingira wezeshi yanayofanywa na Serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu.

“Mkataba tuliousaini na Europian wa mkopo wa Euro milioni 20 ambao ni takribani bilioni 50 za kitanzania utakwenda kuwasaidia wakina mama katika harakati zao za ujarisiliamali.”

Amesema ni wazi kuwa sekta ya ujasiriamali Nchini inahusisha wanawake wengi zaidi Nchini hivyo –KCB itaendelea kuleta huduma bunifu zitakazomlenga mtanzania moja kwa moja.

Pia ameishukuru serikali kwa kuendelea kuiunga mkono sekta binafsi na kutengeneza mazingira ambayo yanawafanya wawekezaji wa nje kuongeza na kuja kuwekeza nchini.

Itakumbukwa kuwa serikali imeendelea kuhamasisha taasisi za fedha Nchini kuunga mkono jitihada za serikali katika kuwainua wajasiriamali nchini wakiwemo wanawake ambapo –KCB imetekeleza hilo.