January 27, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Benki ya Equity yazindua kampeni ya ‘Ishi Kisasa Pesa Mzigo’

Na Jackline Martin,Timesmajira Online

BENKI ya Equity  nchini imesema  itaendelea kuhakikisha inaunga mkono Mipango ya kimaendeleo ya serikali ya kuhakikisha watanzania wengi wanafikiwa na  huduma za kifedha kupitia digital ili  kuachana na fedha taslim ambayo riski yake ni kubwa.

Haya yameezwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Isabella Maganga wakati wa uzinduzi wa kampeni yake ya Ishi kisasa Pesa mzigo inayolenga kuwawezesha watanzania na wafanyabiashara kufanya malipo kwa njia ya kidigitali.

“Njia za kidigitali kwa sasa ni salama zaidi kuliko kutembea na cash na ni nafuu kwa maana ya kwamba hauitumii muda Kama unavyokwenda kwenye tawi kufuata huduma za kibenki lakini pia Gharama zake ziko chini ukilinganisha na njia nyingine zote ambazo unaweza kufanya huduma za kibenki”

Aidha ameongeza kuwa hivi sasa mteja anatakiwa kupata huduma za kibenki popote alipo na si kwenda kupanga foleni kwenye matawi ya benki na kuwa huduma hizo  ni salama  na zinaokoa muda  na gharama kwa mtumiaji.

Aidha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema kupitia Kampeni hiyo kwa sasa wanampango wa kuwafikia Watanzania wengi zaidi kwasababu kila mtanzania anastahili kupata huduma za kibenki ili kuishi kisasa na kuondokana na mzigo wa fedha;

“Kwa kupitia njia hiyo tutawafikia Watanzania walio wengi, kwa sasa tupo zaidi ya milioni 60 na tunashukuru tutakuwa na sensa kwahiyo tutakuja kujua idadi kamili ya Watanzania na wote Watanzania wanahitaji kupata huduma za kibenki kwahiyo kwa kupitia njia za kidigitali tutaweza kuwafikia Watanzania walio wengi na kusababisha kuishi kisasa na kuondokana na mzigo wa fedha”

Kwa upande wake Meneja mkuu kitengo cha malipo wa Equity  Victor Wanjihia amefafanua kuwa  wamekua Wanawezesha wafanyabiashara kutoa huduma za malipo kidigital  kupitia   mfumo  miwili ikiwemo ya  machine, ambazo zinatumia kadi,na mfumo wa E commerce unaowawezesha kupokea malipo yeyote.