LONDON, England
NYOTA wawili wa timu ya Taifa ya England Mason Mount na Ben Chilwell wameondolewa kwenye mchujo wa Kundi D la Euro 2020 leo dhidi ya Jamhuri ya Czech na pia wanaweza kukosa raundi ya 16 baada ya kulazimishwa kujitenga kutokana na COVID 19.
Wawili hao walionekana kuwa na mawasiliano ya karibu na mwenzao wa Chelsea Billy Gilmour, ambaye alipimwa na kukutwa na virusi vya Corona katika sare ya 0-0 dhidi ya Scotland mchezo uliofanyika Ijumaa huko Wembley.
Mount na Gilmour walionekana wakimkumbatia Gilmour wakati wa mazungumzo yao, hivyo kutokana na sababu za kiafya ya Umma England iliona kama wawili hao walionekana kuwa na mawasiliano ya karibu na mchezaji huyo.
Taarifa kutoka Shirikisho la Soka England lmesema “Tunathibitisha kwamba Ben Chilwell na Mason Mount lazima wakae karantini hadi Jumatatu ijayo Juni 28 mwaka huu. Uamuzi huu umechukuliwa kwa kushauriana na Afya ya Umma England.
“Wawili hao wamethibitishwa mara moja kama walikuwa na mawasiliano ya karibu na Billy Gilmour wa Scotland baada ya kupimwa corona na kukutwa nayo kufuatia mechi ya Ijumaa iliyopita.
“Chilwell na Mount watajitenga na kufanya mazoezi mmoja mmoja katika maeneo binafsi kwenye uwanja wa mazoezi wa England St George’s Park, na kikosi kingine kitashuka huko baada ya mechi ya leo jioni dhidi ya Jamhuri ya Czech huko Wembley.
“Tutaendelea kufuata itifaki zote za COVID-19 na serikali ya upimaji wa UEFA, huku tukiwa tumewasiliana sana na PHE.
“Kikosi chote cha England na wafanyakazi walikuwa na vipimo vya mtiririko jana Jumatatu na wote walikuwa hasi, kama ilivyokuwa kwa vipimo vya PCR vya Jumapili mapema vya UEFA. Uchunguzi zaidi utafanywa,” imesema taaifa ya FA.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania