March 8, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bei za mafuta zaendelea kushuka

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Dodoma

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za mafuta zinazotumika kuanzia Septemba 3, 2025, zikionesha kupungua kwa shilingi 36 kwa bei ya petroli na shilingi 23 kwa bei ya dizeli.Kwa mafuta yaliyopokelewa bandari ya Dar-es-Salaam,Tanga na Mtwara mtawalia.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Andilile,amesema bei ya petroli katika soko la dunia imepungua kwa asilimia 0.2,dizeli kwa asilimia 5.5 na mafuta ya taa kwa asilimia 3.5. Vilevile, kwa bei za mwezi Septemba, 2025, wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni umepungua kwa asilimia 3.96.

Gharama za kuagiza mafuta katika bandari ya Dar-es-Salaam zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 20.73 kwa mafuta ya petroli,asilimia 7.75 kwa mafuta ya dizeli na asilimia 2.62 kwa mafuta ya taa.

Hata hivyo katika bandari ya Mtwara hakuna mabadiliko huku katika bandari ya Tanga zimepungua kwa asilimia 12.66 kwa mafuta ya petroli na asilimia 12.66 kwa mafuta ya dizeli.

Aidha, wafanyabiashara wanakumbushwa kuuza mafuta kwa bei zilizoidhinishwa na EWURA na yeyote atakayekiuka agizo hili atachukuliwa hatua za kisheria.