Na Hamisi Miraji, Timesmajira Online
MWANAMUZIKI maarufu wa Hip pop nchini Marekani, Snoop Dogg ameamua kuacha kuvuta bangi kwa kile anachodai umri wake unazidi kumtupa, hivyo anahitaji kubadilika.
Snoop amepost muda si mrefu katika ukurasa wake wa Instagram nia yake hiyo. Snoop amesema maamuzi ya kuacha kuvuta bangi yanatokana na mtoto wake mkubwa aitwaye Corde kuwa baba wa mtoto Zion, hivyo anajiona kuwa ameshakuwa mzee kwa hiyo matumizi ya kilevi hicho kwa sasa sio sahihi kwake.
Rapa huyo mwenye umri wa miaka 52 anadai kwa sasa jamii inayomzunguka iheshimu maamuzi yake licha ya wengi wao kupata mshtuko kwani alikuwa amebobea katika uvutaji wa bangi.
“Kuwa babu imenibadilisha sana, kwa sababu nataka kuona wajukuu zangu wakiwa waniona babu yao nipo katika mwenendo mzuri hivyo lazima nichukue tahadhari mapema ili wasinielewe vibaya,” ameseam Snoop.
Snoop ni baba wa watoto wanne, Corde (28), Cordell (26), na Cori (23) kutoka kwenye ndoa yake iliyodumu takribani miaka 25 huku mtoto wake qa nne Julian mwenye miaka 25 akizaa na mpenzi wake wa zamani Laurie Holmond.
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA