MUNICH, Ujerumani
KLABU ya Bayern Munich imekamilisha usajili wa Tanguy Kouassi kutoka Paris Saint-Germain, kwa mkataba wa miaka minne kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo kwenye Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga.
Kouassi, mwenye umri wa miaka 18 raia wa Ufaransa, ameichezea PSG michezo 13, na pia ndiye mchezaji mdogo zaidi kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa klabu hiyo akiwa na umri wa miaka 17, miezi sita na siku tano.
Mchezaji huyo anayecheza nafasi ya ulinzi na kiungo amejiunga na wachezaji wenzake wa Ufaransa kama Kingsley Coman, Benjamin Pavard, Lucas Hernandez, Corentin Tolisso na Michael Cuisance.
More Stories
Naibu Waziri wa Fedha abariki ujio mpya wa Bahati Nasibu
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes