Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MKUU wa Wilaya ya Korogwe na Miss Tanzania 1998 Basilla Mwanukuzi, ameahidi kufanya mambo makubwa katika Wilaya hiyo mara atakapokabidhiwa ofisi siku chache zijazo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.
Akitoa ahadi hiyo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Basilla amesema, anatarajia kuanza majukumu yake rasmi mara tu yatakapofanyika makabidhiano rasmi ya ofisi siku chache zijazo.
“Nina shauku kubwa ya kuwatumikia wana Korogwe nikishirikiana na watendaji wa ofisi ya Mkuu wa wilaya, watendaji wa halmashauri , wabunge , tukiongozwa na Mkuu wetu wa Mkoa Adam Malima, viongozi wa Chama chetu cha mapinduzi wadau mbali mbali na ushirikiano mkubwa wa wananchi, lengo kuu ikiwa ni kuwatumikia wananchi , kuwaongoza ili nao waweze kunufaika na kuwa na ustawi katika nchi yao .
“Adhma ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kuchapa lazi na kuhakikisha adhma ya maisha bora kwa kila Mtanzania iweze kuendelea kutumia. Kua karibu na wananchi kujua kero zao na kuzipatia ufumbuzi , ufumbuzi wa kudumu.
“Kuwaamsha waweze kuchangamkia fursa. Wilaya ya Korogwe ina fursa nyingi za uwekezaji, ina ardhi yenye rutuba ya kustawisha mazao mbali mbali ya chakula na biashara sambamba na mifugo. Kuna zao la Mkonge ambalo linautajiri mkubwa. Kuna vivutio vya utalii vya kuwekeza. Fursa za kuwekeza katika huduma za Afya Elimu, Mashule na Michezo., kuna bomba la gesi linalopita katika ukanda huu wa mkoa wa Tanga, kunafursa ya kuhudumia wasafiri .
“Ikumbukwe Korogwe ni kitovu cha kupitisha wasafiri wa ndani na nje ya nchi na fursa nyingine nyingi tutakazokua tunazitangaza kwa wananchi. Kwa hakika Mungu atatusimamia katika kuyatekeleza haya. Karibu sana Korogwe,” amesema Basilla.
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio