
Na Mwandishi Wetu, Mkalama.
Abiria kadhaa wamenusurika kifo baada ya basi la kampuni ya Ester walilokuwa wakisafiria kutoka mjini Singida kwenda kijiji cha Ibaga, mpakani mwa Mkoa wa Singida na Simiyu, kupata ajali na kupinduka katika kijiji cha Isene, Wilayani Mkalama.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka eneo la tukio, ajali hiyo ilitokea Machi 5, 2026, majira ya saa 6 mchana katika eneo la mpaka kati ya vijiji vya Isene na Matongo.

Diwani wa Kata ya Matongo, Erasto Linza, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa ilisababishwa na hitilafu ya mfumo wa usukani baada ya kifaa cha kufunga usukani kuharibika, hali iliyosababisha dereva kushindwa kulidhibiti basi hilo.
Amesema kuwa hakuna kifo na kwamba abiria wote wako salama na tayari basi hilo lilirekebishwa na kuendelea na safari baada ya tukio hilo.


More Stories
Kihongosi amtaka mkandarasi kuwalipa vibarua stahiki zao
DC Mbozi afuturisha wananchi, asisitiza mshikamano na Umoja.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Nina imani mubna utendaji kazi wa ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria