November 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bashungwa ataja vigezo vitakavyotumika kupima Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Innocent Bashungwa amesema kuwa Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Wilaya watapimwa kutokana na utendaji kazi wao wa kuhakikisha wanatatua kero za wananchi.

Akiongea na viongozi wa Mkoa wa Njombe leo Waziri Bashungwa amesema moja ya kigezo cha kuwapima Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya ni kasi ya ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri, amewaagiza kuhakikisha wanaongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato

Ameongeza kuwa fedha nyingi zinatolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo hivyo ni wajibu wa viongozi hao kuhakikisha wanasimamia matumizi ya fedha hizo, hivyo nitoe wito kwa Wakurugenzi Wakuu wa Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia matumizi ya fedha hizo kwa uaminifu.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametuamini vijana katika kumesaidia kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi hivyo Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya tusimuangushe na Mimi nikiwa ni Waziri mwenye dhamana sitakubali kumuangusha” amesisitiza Waziri Bashungwa

Waziri Bashungwa amesisitiza Wakurugenzi kuhakikisha wanajibu hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa asilimi 100 na kuhakikisha fedha zinazokusanywa zinawekwa benki kwa wakati na kuacha tabia ya kutumia fedha mbichi,

Ameongeza kuwa kigezo kingine ni utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu amewataka kuhakikisha fedha inayotolewa inaenda kwenye miradi yenye tija ya kuwasaidia waliopewa, amewataa Viongozi hao kutoa ushauri wa namna bora ya kukusanya fedha zilizotolewa.

Aidha amewaagiza wakuu wa Mikoa wote nchini kuhakikisha wanasimamia utoaji wa mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na kuhakikisha fedha hizo zinaenda kwenye miradi yenye tija na kama kuna ujanja unaofanywa na Halmashauri au idara inayoshughulikana mikopo wafuatilie na kutoa taarifa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuwa hicho piano kigezo kingine cha kuwapima Wakurugenzi katika Halmashauri kwa kuangalia wanasimamia vipi utoaji wa mikopo ya asilimia kumi