Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, limempongeza mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Khamis Katimba kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ukusanyaji wa mapato, ustawi wa wananchi na uboreshaji wa utawala bora.
Kwa niaba ya baraza hili, pongezi hizo zilitolewa na Shija Joseph Luyobya, Diwani wa Kata ya Bulyanhulu katika Kikao cha Baraza cha robo ya tatu.
Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kilipokea na kujadili taarifa kutoka kwa kmati mbalimbali za kudumu ambapo wajumbe wa baraza hilo, wakimpongeza Katimba kutokana na ubunifu wake katika utendaji.
“Mwenyekiti, sisi madiwani kwa dhati kabisa tunampongeza sana Mkurugenzi Mtendaji wetu wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kwa utendaji bora wake katika kuwahudumia wananchi, kutekeleza miradi ya maendeleo, kuboresha utawala bora, upatikanaji wa Hati safi 2022/203
“Zaidi tunampingeza kwa kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato ambapo mpaka sasa amekusanya 98% wakiwa wamevuka lengo la serikali kabla ya Juni 30, 2024,” alisema Luyobya.
Kwenye kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, AbdulKadir Mfilinge aliwakunbusha wafanyakazi na watendaji katika hamashauri hiyo kuhakikisha wanaondoa dosari zote kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani.
Pia aliwataka kutekeleza agizo la serikali kwa kutembelea miradi yote na kujibu kero za wananchi.
Kwenye kikao hicho kilichofanyika kwa siku mbili wiki hii, Mfilinge alisema kikao kilichofanyika kati ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), na wakurugenzi wote nchini, Kibaha mkoani Pwani mapema wiki hii, kimeagiza pamoja na mambo mengine, watendaji kufanya maandalizi ya uchaguzi pia kwenda kwa wananchi kusikiliza na kutatua kero zao.
“Kikao kimeagiza kufanya maandalizi ya chaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu kwa kuondoa dosari zote kabla ya uchaguzi, usimamizi wa miradi, utatuzi wa kero, kutembelea miradi,
ukusanyaji wa mapato sambamba na uondoaji wa migongano baina ya wenyeviti na wakurugenzi, alisema Mfilinge.
Alisema, Mwaka wa Fedha 2024/2025 Serikali itapeleka fedha nyingi kwenye halmashauri hiyo ili kutekeleza miradi mbalimbali katika Sekta za Elimu na Afya.
“Fedha hizo zitakapofika, ninaomba Mamlaka za Serikali za Mitaa kuzisimamia kikamilifu,” alisema.
Akizungumzia maendeleo ya Msalala, Mfilinge alimpongeza mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Khamis Katimba kwa kuwezesha kupata hati safi.
Na kwamba, miongoni mwa juhudi anazofanya mkurugenzi huyo ni pamoja na hufanya vikao kazi
vingi ngazi za Vijiji, Kata na Halmashauri ili kuhakikisha dhana ya utawala bora inafanikiwa.
“Hakika mkurugenzi wetu yupo makini, hatua anazochukua zinaifanya halmashauri yetu kukimbia kwa kasi kubwa, tunakwenda naye vizuri sana,” alisema.
Diwani wa Kata ya Bulyanhulu, Shija Luyombya alisema ili halmashauri hiyo ifanikiwe zaidi, aliwaomba watendaji kushirikiana na mkurugenzi huyo kwa kuwa, ana malengo chanya na Msalala.
“Tumeona kasi yake na sisi wote ni mashahidi katika hili, tunapaswa tumsaidie zaidi kwa kuwa, ameonesha utayari kwa vitendo,” alisema.
Katika kika hicho Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya menejimenti, ufuatiliaji na ukaguzi, Ibrahim Makana alishauri kuongeza kasi ya makusanyo ya mapato.
“Kumbukeni kutenga fedha za mafunzo mara baada ya uchaguzi kwa viongozi, shughuli zinazoandikwa ziweze kupimika na hakikisheni makusanyo ya 60% ya miradi ya maendeleo na 10% ya wanawake, vijana, walemavu na watoto zinapelekwa kama ilivyopangwa,” alisema.
Aliagiza kwamba, fedha zote zinazokusanywa kupitia mfumo wa TAUSI zipelekwe benki siku hiyo hiyo zilipokusanywa ili kuondoa mashaka yasizokuwa na ulazima.
Baraza hilo limehitimishwa jana kwa wajumbe kutaka mapato kukusanywa kwa namna yoyote lakini kwa kufuata sheria.
Pia madiwani walishairi mawakala kubadilishwa mageti mara kwa mara kwa lengo la kuondoa mazoea sambamba na kufanya doria.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi