Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online- Kigoma
WAKALA wa Barabara za Mjini na Vijijini(TARURA), Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma,imetakiwa kuweka kipaumbele katika barabara za vijijini zilizoathiriwa na mvua.
Hayo yameelezwa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Augustine Mbanga,wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo wa kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kipindi cha robo ya tatu kuanzia Januari hadi Machi 2026.
Ambapo amesema Serikali imeendelea kuleta maboresho katika sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara, elimu, afya na huduma za maji, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa kipaumbele kwa barabara ambazo zimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na mvua.
“Naipongeza Serikali kwa kuendelea kufanya kazi kubwa ya kuboresha maisha ya wananchi kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Hivyo ni muhimu kuendelea kuimarisha barabara za vijijini ili wananchi waweze kufanya shughuli zao kwa urahisi zaidi,”amesema Mbanga.
sanjari na hayo ametumia fursa hiyo kumpongeza Mkurugenzi , Mwl. Chiriku Chilumba pamoja na wataalam wa halmashauri hiyo,kuongeza kiwango cha makusanyo ya mapato ya ndani yaliyowezesha kuimarisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma kwa wananchi kwa ufanisi na wakati.
Kwa upande wake Dorah Buzaile, aliyemwakilisha Katibu Tawala wa Wilaya hiyo,amesema Serikali itaendelea kuhakikisha changamoto zinazowakabili wananchi zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati ili kuongeza ustawi wa jamii.
Huku akiwasisitiza Madiwani kuendelea kushirikiana na wataalam ili kwa pamoja changamoto za wananchi ziweze kupatiwa ufumbuzi.
Mkutano huo umehudhuriwa na wataalam kutoka TARURA, TANESCO, RUWASA pamoja na wataalam wa halmashauri na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.

More Stories
Bulaya:Bil.9 zimetengwa Bunda kwaajili ya Maji
Wakazi kunduchi kunufaika huduma za Yas, Mixx
IFC, BII na Norfund zaipa NMB ufadhili wa Dola Mil. 180