Na Angela Mazula TimesMajira Online
UPUNGUFU wa vifaa tiba katika Zahanati Kata ya Rasbura iliyopo Manispaa ya Lindi umesababisha huduma ya uzazi kuendelea kutolewa katika mazingira magumu hali ambayo inawalazimu wakazi wa kata hiyo kutumia gharama kubwa kufika katika hospital ya Rufaa ya Sokoine mkoani humo.
Zahanati hiyo yenye muuguzi mmoja na daktari mmoja inahudumia wakazi hao kwa muda mrefu, hivyo wameiomba Serikali kupeleka vifaa tiba katika jengo la mama na mtoto ili huduma za afya ikiwemo uzazi zifanyike katika mazingira rafiki ukilinganisha na huduma zinazotolewa kwa sasa.
Banki ya NMB tawi la Lindi, limesikia kilio hicho na kusaidia baadhi ya vifaa ikiwemo Mashuka 20, Delivery kit set (04) Vitanda vya wagonjwa 03, Kitanda Cha kujifungulia 01 , (Making tosh) pamoja na mipira ya kujifungulia.
Akizungumzia hilo, Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga mara baada ya kupokea vifaa hivyo vilivyokabidhiwa kwake akiwepo mbunge wa jimbo la lindi Mjini Hamida, ameishukuru Benki ya NMB kwa kurudisha sehemu ya faida kwa kutoa msaada wa vifaa tiba mbalimbali vya zahanati hiyo vyenye thamani ya Shs milioni 5.
Naye Mbunge wa Jimbo hilo Hamida Abdallah amesema,” nimefurahishwa na uharaka uliofanywa kutatua changamoto za wanawake ili kupata huduma za afya kwa ukaribu kama matakwa ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi,’’ amesema.
Naye Meneja wa huduma kwa Wateja Benki ya NMB Lindi, Eyya Ngolo amesema, banki hiyo hivi karibuni imetoa misaada kama hiyo katika zahanati ya Mtama na Kituo cha afya Pangaboi kwa kuamini kuwa afya na elimu ni msingi wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa, hivyo hiyo ni njia ya kurejesha faida kwa wananchi.
Hata hivyo amewataka wadau wengine kusaidia kukarabati jengo la kujifungulia ambalo kwa sasa ni chakavu linalohitaji jumla ya Shilingi milioni kwa ajili ya kubadili bati 30, milango na miundombinu mingine ili wanawake wengi zaidi waweze kujifungulia katika zahanati hiyo.
Kwa sasa Zahanati hiyo ina uwezo wa kupokea wagonjwa 157 wanawake, lakini wengi wanakwenda hospitali ya mkoa kutokana na zahanati hiyo kuwa na ufinyu wa nafas, uhaba wa vifaa na huduma duni.
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano