Na Patrick Mabula , Kahama.
BALOZI wa Baba Mt.Papa Francis nchini, Askofu Mkuu Marek Solczynski, ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuruhusu watu kwenda kusali katika nyumba za ibada ili kumuomba Mungu katika kipindi hiki cha janga la ugonjwa wa Corona.
Askofu Mkuu Solczynski amemshukuru Rais John Magufuli kwa busara yake kuruhusu watu kusali katika nyumba za ibada ili kumuomba Mungu, hivyo amewataka kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Serikali kwa ajili ya kujikinga na maabukizi ya ugonjwa wa Corona.
Akizungumza jana wakati wa Misa ya kubariki mafuta yanayotumika katika ubatizo wa waumini pamoja na kurudia ahadi za upadri iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Karoli Lwanga Parokia ya Kahama Mjini, Askofu Solczynski alisema pamoja na janga la ugonjwa wa Corona, lakini anaishukuru Serikali kwa kuruhusu watu kusali makanisani.
“Kipindi hiki kuna janga la ugonjwa wa Corona ulioikumba dunia, lakini kwa kutabua umuhimu wa watu kwenda kanisani kusali na kumuomba Mungu ni jambo kuishukuru Serikali kwa kuruhusu watu kusali.
Jambo la muhimu sana ni kufaata maelekezo ya kujikinga na maabukizi ya virusi vya COVID -19,” alisema Askofu Solczynski .
Askofu Solczynski aliwataka waumini kusali na kumuomba Mungu ili aweze kutuponya na janga la Corona ambalo limeikumba dunia.
“Kutokana na janga la virusi vya Covid-19 Baba Mtakatifu Papa Francisco huko Vatican katika Viwanja vya Basirika vya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro ataadhimisha Misa ya Pasaka peke yake kwa sababu ya ungonjwa wa Corona,” alisema Balozi huyo.
Naye Paroko wa Kanisa Kuu la Padri Sarvatore Guerera, aliwataka waumini wanapokwenda kanisani kufuata maelekezo yaliyotolewa na Serikali kupitia wizara ya afya pamoja na yale yaliyoelekezwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) katika kujikinga na maabukizi ya ugonjwa wa Corona.
Balozi wa Vatican yupo Jimbo Katoliki la Kahama kwa ziara ya kichungaji kwa wiki hii yote ya Juma Kuu la Mateso ya Yesu kusali na waumi hadi atakapoadhimisha Misa ya cha Pasaka.
More Stories
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua
Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa
Vikundi Ileje vyakabidhiwa mikopo ya asilimia 10, DC Mgomi avipa somo