January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Balozi Sokoine ateta na ujumbe wa PanAfrican Energy

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Kampuni ya Panafrican Energy Tanzania Ltd katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Ujumbe wa Kampuni ya African Energy Tanzania Ltd umeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Andrew Hanna ambapo viongozi hao pamoja na mambo mengine, wamejadili fursa za biashara na uwekezaji katika sekta ya gesi.