December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Balozi Siwa aapishwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online DSM

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Ali Idi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Balozi Siwa ameapishwa leo Agosti 28, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam akichukuwa nafasi ya Said Hussein Massoro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.