April 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Balozi Shiyo amewasilisha hati za utambulisho kwa Umoja wa Afrika

 

Na Mwandishi  wetu,timesmajira,online

BALOZI  wa Tanzania nchini Ethiopia na
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Afrika,Innocent Eugene
Shiyo  amewasilisha Hati zake za Utambulisho kwa, Mwenyekiti wa
Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Faki Moussaka Mahamat.

Akizungumza katika hafla ya kupokea hati
hizo,Mwenyekiti wa Kamisheni hiyo,Mahamat alimpongeza Balozi Shiyo kwa
kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan,  kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa
Tanzania kwenye Umoja wa Afrika.
amesema anamtakia
 heri katika utekelezaji wa majukumu yake katika umoja huo.

Akizungumzia mambo ambayo wamekubaliana
katika kushirikiana kwao ni pamoja na  kusimamia utekelezaji wa masuala ya
kipaumbele ya Umoja wa Afrika hususan juhudi za kupambana na UVIKO-19 ikiwemo
upatikanaji na utengenezaji wa chanjo za ugonjwa huo barani Afrika pamoja na
mikakati ya kunasua uchumi wa Afrika dhidi ya athari za UVIKO-19.

“Tumekubaliana  kushirikiana katika
kutekeleza miradi ya kipaumbele ya Umoja wa Afrika yenye lengo la kuimarisha na
kukuza Mtangamano wa Afrika hususani ujenzi wa miundombinu ya uchukuzi,
kuboresha mazingira ya biashara kupitia Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika
(AfCFTA) na juhudi za uimarishaji wa hali ya amani, usalama na utulivu barani
Afrika,”
amesema na kuongeza

“Tumekubaliana  kuhusu umuhimu wa
utekelezaji wa mchakato mabadiliko ya kitaasisi ndani ya Umoja wa Afrika ili
kuboresha utendaji wa umoja huo,”
amesema  Mwenyekiti
Mahamat

Kwa upande wake ,Balozi Shiyo alizungumzia
kwa undani umuhimu wa kutekeleza maazimio mbalimbali ya Wakuu wa Nchi na
Serikali ya kuwezesha lugha ya  Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha za kikazi
za umoja wa Afrika.

Mwenyekiti,Mahamat amemuhakikisha  Balozi Shiyo kuwa ataunga 
mkono ombi la Tanzania kutaka lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha za
kazi za Umoja wa Afrika.

Mwenyekiti  Mahamat ametumia fursa hiyo kutoa  salamu za shukurani kwa
Rais  Samia kwa kumwalika kushiriki Maadhimisho ya Miaka 60 na zaidi kwa
kukubali kuonana naye Disemba 10, 2021.

Mwenyekiti  Mahamat amesema alipata fursa ya kumwelezea, Rais Samia
 kuhusu maeneo ya mbalimbali kipaombele ndani ya Umoja wa Afrika na Afrika
kwa ujumla.