December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Balozi Nchimbi aongoza mazishi ya Mama mzazi wa Liongo

Na Agnes Alcardo,TimesmajiraOnline,Dar

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi, amewaongoza mamia ya wananchi wakiwemo viongozi wa Chama cha CCM na Pinzani,Wakurugenzi wa Taasisi za Kiserikali na Wanahabari katika mazishi Zainab Nkya(75) ambaye ni Mama Mzazi wa Ofisa Mwandamizi Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo,CCM Taifa, Aboubakary Liongo.

Zainab ambaye alifariki Septemba 30, mwaka huu Katika Hospitali ya Rabininsia iliyopo Jijini Dar es Salaam, mazishi yake yameongozwa na Imamu Msaidizi wa Masjid Maamur Upanga, Sheikh Ramadhan Koba.

Ambapo amezikwa katika Makaburi ya Kisutu, yaliyopo katika Kata ya Kisutu, Wilaya ya Ilala, yamehudhuriwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, ambaye pia ni Msemaji wa Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba.

Wengine waliohudhuria katika mazishi hayo ni Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile, Mkurugenzi wa Baraza la Habari (MCT), Ernest Sungura, Mkurugenzi Mtendaji wa Vyombo vya habari vya CCM, Shaban Kisu na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu.