January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Balozi Dkt. Nchimbi leo Kuunguruma Singida

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online

ZIARA ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, kuanza leo katika mikoa mitano huku mmoja ukiwa wa Kanda ya Kati na minne ikiwa katika Kanda ya kaskazini, yenye lengo la kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa chama hicho ya mwaka 2020/2025.

Katika ziara hiyo Dkt. Nchimbi ataambatana na Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla, pamoja na Katibu wa NEC – Mambo ya siasa na uhusiano wa kimataifa, Rabia Hamid.

Ziara hiyo itahusisha Mkoa wa Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na kumaliza katika Mkoa wa Tanga, Juni 9 2024.

l