Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Michael A. Battle Agosti 14, 2024 ametembelea TRA na kufanya mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda katika ofisi za TRA Makao Makuu jijini, Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao Kamishna Mkuu alimuhakikishia Balozi huyo kuendeleza ushirikiano Kati ya TRA na wawekezaji wa Marekani na wa nchi nyingine pamoja na kuzitafutia ufumbuzi changamoto za kikodi ambazo wawekezaji kutoka marekani wanakumbana nazo ili waendelee kuwekeza Tanzania na kuinua uchumi wa nchi.
More Stories
Waislamu wamuombea dua Rais Samia,wasisitiza umoja
Samia: Serikali imejifunza somo kuporomoka ghorofa
Wanachama CCM Kata ya Rujewa wajitokeza kufanya usafi kituo cha afya