Na Joyce Kasiki,Timesmajira online, Dodoma
MTENDAJI Mkuu wa Mahakama Prof.Elisante Ole Gabriel ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti ya mahakama kutoka shilingi bilioni 155 mwaka huu wa fedha unaoishia Juni 30 hadi kufika shilingi bilioni 241.6 mwaka 2024/2025.
Akizungumza kuhusu miaka mitatu ya Dkt.Samia katika taasisi hiyo ya Mahakama Prof.Ole Gabriel amesema hatua hiyo inaonesha ni jinsi gani ambavyo serikali inathamini na kutambua majukumu yanayofanywa na taasisi hiyo .
Kufuatia hali hiyo Mtendaji Mkuu huyo wa Mahakama amesema,kumekuwa na maboresho makubwa katika taasisi hiyo ikiwemo katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Habari (TEHAMA) ambayo yamerahisisha utendaji kazi wa mahakama lakini pia kuondoa usumbufu kwa wananchi kuhudhuria mahakamani kwa shughuli mbalimbali huku akisema Mahakama ni taasisi ya kwanza ya umma ambayo ina matumizi ya hali ya juu ya mtandao.
“Hivi sasa tunayo mifumo ambayo inarahisisha utendaji kazi wa mahakama,kwa mfano tunao mfumo wa Ofisi Mtandao ambapo Mashauri mengi sasa yanaendeshwa kwa njia ya mtandao
“Ofisi mtandao tayari inafanyika ndani ya mahakama na inawezesha watu kufanya kazi bila kuwa ndani ya ofisi zao,hata wakiwa nje au ndani ya nchi kazi zinaendelea kufanyika.amesema na kuongeza
“Na Mfumo huu unatembelewa na wadau kwa zaidi ya asilimia 82.4 na nchi inayotufuatia inatembelewa na wadau kwa asilimia 2.7 .”amesisitiza
Vile vile amesema upo mfumo wa TTS ambao husaidia kufanya ukalimani wa hukumu zote,unafanya udukuzi,ambapo wenyewe unaweza kuandika lugha ya kingereza au kiswahili.
Aidha amesema Mahakama imeanzisha kituo cha kupiga simu ‘ call center ‘ kwa ajili ya kupata mrejesho wa taarifa kwa namna gani wananchi wanaridhika na utendaji wa mahakama na kurudisha mrejesho ili kuzifanyaia kazi changamoto zilizobainishwa na wananchi.
Kwa mujibu wa Prof.Ole Gabriel kutoka na mifumo iliyopo katila mahakama wananchi wanaweza kufungua kesi,kujua tarehe ya kesi yake na hata kupata nakala ya hukumu kwa njia ya mtandao.
Hata hivyo amesema licha ya kazi kurahisishwa na mifumo lakini bado kuna changamoto ya wanabchi kutaka kufika mahakamani kwa jambo ambalo lingeweza kufanyika kupitia mtandao.
Aidha amesema taasisi hiyo inaendelea kuelimisha umma kupitia wasanii na vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo kufanya kipindi katika radio na televisheni kuhusu matumizi ya mifumo hiyo ili wananchi waweze kuitumia ipasavyo.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria