April 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bahati Nasibu ya Taifa, Selcom zashirikiana ununuzi wa tiketi

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

BAHATI Nasibu ya Taifa, imetangaza rasmi ushirikiano na mtoa huduma kinara wa malipo kwa njia ya simu nchini Selcom Tanzania, ili kuhakikisha Watanzania wanashiriki katika michezo ya bahati nasibu kwa urahisi.

Ushirikiano huo utarahisisha upatikanaji,
ununuzi na ulipaji wa tiketi kwa urahisi na usalama nchini kote.

Ushirikiano huo na Selcom Tanzania, ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa Bahati Nasibu
ya Taifa inawafikia Watanzania wote nchini.

Kwa kutumia miundombinu madhubuti ya malipo
ya Selcom, Wachezaji wataweza kushiriki katika michezo ya bahati nasibu kupitia USSD codes,
Kuhamisha kutoka benki, mawakala wa selcom huduma ambao wapo zaidi ya 30000 nchi
nzima,na vituo vya selcom 10 vilivyopo maeneo mbalimbali hapa nchini.

Pia, washiriki wa bahati nasibu ya taifa wataweza kununua tiketi na kupokea malipo ya ushindi kupitia majukwaa ya fedha kwa njia ya simu, USSD, hamisho kutoka benki, vituo vya malipo ya Selcom, na miamala ya kidijitali.

Aidha, upatikanaji wa Selcom katika taasisi mbalimbali za kifedha utahakikisha kuwa hata wale wanaoishi maeneo yasiyofikika kiurahisi wanaweza kushiriki kikamilifu katika michezo ya bahati nasibu ya taifa.

Mkurugenzi wa ITHUBA Tanzania, Kelvin Koka, ameelezea umuhimu wa ushirikiano huo
na Selcom Tanzania, amesema ni hatua kubwa katika sekta ya michezo.

“Hii ni ni hatua kubwa katika sekta ya michezo ya kubahatisha nchini, kwa kushirikiana na Selcom, tutahakikisha kuwa Bahati nasibu ya Taifa itakapozinduliwa kila Mtanzania bila kujali mahali alipo nchini, ataweza kushiriki kikamilifu katika michezo mbali mbali ya kusisimua ya bahati nasibu,” amesema Koka.

Amesema, Bahati nasibu ya Taifa si michezo ya kubahatisha tu bali pia ni chombo cha maendeleo ya taifa Sehemu ya mapato yatokanayo na mauzo ya tiketi za bahati nasibu yatatengwa kwaajili ya miradi muhimu kama vile kuendeleza michezo ya vijana chipukizi, na sekta nyingine zinazo igusa jamii.

Aidha, amesema Ushirikiano huo na Selcom utakuwa na mchango mkubwa katika kuongeza ushiriki wa umma, hatimaye kuongeza mchango wa pato la Taifa kupitia miradi hiyo.

“Usalama ni nguzo kuu ya ushirikiano huu, ambapo kupitia teknolojia bora ya Selcom washiriki
wataweza kununua tiketi, kupokea malipo kidigitali kwa usalama ambao utazuia udanganyifu
wa aina yoyote,” amesema.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa ushirikiano huu, Shumbana Walwa, Mkuu wa idara
ya Masoko wa Selcom Tanzania amesema,

“Ushirikiano wetu na Bahati nasibu ya Taifa ya
Tanzania unalenga kurahisisha ushiriki katika michezo ya kubahatisha kwa kila Mtanzania.

“Kupitia miundombinu yetu imara ya malipo, tutahakikisha kuwa mara tu Bahati nasibu ya Taifa itakapozinduliwa, wachezaji wataweza kushiriki kwa urahisi kupitia njia ambazo tayari
wanaziamini na kuzitegemea.

“Tumejidhatiti kutoa huduma ya malipo salama, bora, na ya kuaminika ili kuongeza urahisi wa upatikanaji wa michezo ya bahati nasibu na ushiriki,” amesema.

Kwanzia sasa, Bahati nasibu ya Taifa ya Tanzania na Selcom wataendelea kushirikiana kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata uzoefu wa kusisimua wa michezo ya bahati nasibu itakayopatikana katika jukwaa la Bahati nasibu ya Taifa, kwa usalama na uwazi wenye manufaa kwa watu binafsi na taifa kwa ujumla.