November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Baba atuhumiwa kujaribu kumbaka binti yake

Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza

Mwanaume mmoja aitwaye Godbless Mushi,wenye umri wa miaka 39, mfanyabiashara wa kuuza vifaa vya magari na mkazi wa Shibula, wilayani Ilemela anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa tuhuma ya kujaribu kumbaka mtoto wake wa kike.

Mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa kutokana na taratibu za kimaadili, mwenye umri wa miaka 5, mwanafunzi, wa chekechea.

Akizungumza jijini hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa,ameeleza kuwa Jeshi hilo linaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo.

Ambaye ana tuhumiwa kutenda kosa hilo mnamo Aprili 02,2023 majira saa 4(22:00)usiku, Mtaa na Kata ya Shibula Wilaya ya Ilemela, mtoto huyo akiwa amelala chumbani kwenye kitanda cha wazazi wake, wakati mama yake mzazi akiwa anaendelea na shughuli za kawaida ndani ya nyumba yao, ndipo mwanaume huyo alipata nafasi ya kujaribu kumfanyi mtoto wake vitendo vya udhalilishaji wa kingono.

Aprili 3,2023 majira ya saa 3 na dakika 40(09:40)asubuhi , tukio hilo la kikatili liliripotiwa kituo cha Polisi kirumba na kwa haraka Askari wa Dawati la Jinsia walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.

Ambapo walimfikisha kituo cha Polisi Kirumba wilayani Ilemela ambapo ameshikiliwa na anaendelea kuhojiwa kwa kitendo cha uzalilishaji wa kingono alichokifanya kwa mtoto wake wa kumzaa.

Mutafungwa ameeleza kuwa uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea kwa kuwahoji mashahidi na kumfanyia binti huyo uchunguzi wa kitaalamu.

“Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto linaendelea kushughulikia tukio hili kwa kushirikiana na Ofisi ya Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mwanza na upelelezi utakapo kamailika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani,”ameeleza Mutafungwa.

Hata hivyo ameeleza kuwa jeshi hilo linaendelea kutoa wito kwa wananchi kutofumbia macho vitendovya ukatili wa kijinsia kwa watoto na watu wengine vinavyofanyika nyumbani.

Aidha, linawahimiza kuendelea kuyafichua matendo hayo kwa Jeshi la Polisi kupitia Madawati ya Jinsia na Watoto yaliyopo kwenye vituo vya Polisi iliwanaofanya matendo hayo waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.