Na Moses Ng’wat, Timesmajira Online,Songwe.
WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso, amemuagiza Mkurugenzi wa Idara ya Usambazi Maji Vijijini ,Joyce Msiru kwa kushirikiana na watendaji wengine katika Wizara hiyo kuanza mara moja mchakato wa kuunda mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mkwajuni ili kurahisisha utendaji na kufikisha huduma ya maji kwa wananchi.
Ametoa agizo hilo, Julai 31,mwaka huu katika siku yake ya kwanza ya ziara ya siku mbili mkoani hapa mara baada ya kupokea taarifa ya hali ya upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Songwe.
Katika taarifa hiyo ya upatikanaji wa maji ilieleza kuwa Kata za Mkwajuni na Saza ambazo zina idadi ya wakazi wasiopungua 40,000 hivyo kunahitajika msukumo wa ziada wa upatikanaji wa maji.
Kutokana na hali hiyo, Waziri Aweso amesema kwa kuanzia Wizara itapeleka kiasi cha milioni 500 ili kuanzisha mamlaka hiyo ikiwemo na shughuli zingine.
” Mkurugenzi wa idara ya usambazi maji vijijini ‘Msiru” pamoja na viongozi wa Ruwasa Mkoa mnatakiwa kubaki hapa ili kuanza mchakato wa kuundwa mamlaka hii ya Mkwajuni ambayo itahudumia miji ya Mkwajuni na Saza,”amesisitiza Waziri Aweso.
Kiongozi mwingine aliyetakiwa kubaki ili kufanikisha zoezi hilo ni Mkurugenzi wa Ufundi toka RUWASA Makao Mkuu Mhandisi Mengo Ndele, wakisaidiwa na viongozi wengine wa Ruwasa Mkoa na Wilaya.
“Hii ni awamu yangu ya pili kuja Wilaya ya Songwe nimeona mabadiliko makubwa mji umechangamka na naona pilikapilika za biashara ni nyingi, kwa hali hiyo uhitaji wa mamlaka ya maji ni mkubwa,” amesema Aweso
Aidha, Waziri Aweso amesema kuwa Wizara yake imefanya kazi kubwa ya kuweka miundombinu ya maji wilayani humo ambapo kati ya vijiji 43 vilivyopo, vijiji 41 tayari vimewekewa miundombinu hiyo.
Katika hatua nyingine, Waziri Aweso alimuagiza Meneja wa RUWASA Mkoa wa Songwe Mhandisi Charles Pande kutumia milioni 500 toka fungu la uendeshaji ili kununua magari matatu ambayo moja lipelekwe wilayani Songwe kwa ajili ya usimamizi.
Awali Mkuu wa Wilaya hiyo Solomon Itunda akiwasilisha taarifa ya wilaya amesema halmashauri ya wilaya hiyo imetenga zaidi ya milioni 526 hivyo kuwa na upungufu wa bilioni 1.5 ili kuimarisha upatikanaji wa maji katika Kata za Mkwajuni na Saza.
Mbunge wa Songwe Philpo Mlugo alimwambia Waziri Aweso kuwa utendaji wake umesaidia Wilaya yake kupata miradi mingi ya maji na hivyo kupunguza kero ya ukosefu wa maji ilivyokuwa inawakabili wananchi ambao walikuwa wakipata maji ya visima ambayo pia yana harufu ya magadi.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi