January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Auawa kwa kushambuliwa na tembo

Na Steven Augustino,TimesMajira online,Namtumbo

MKAZI wa Kijiji cha Luhangano kata ya Mputa Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma aliyetambulika kwa jina la Issa Ajali amefariki baada ya kushambuliwa na kundi la Tembo.

Taarifa za tukio hilo zinaeleza kuwa marehemu alikutwa na mkasa huo wakati akijaribu kuwafukuza Tembo hao ambalo walivamia shamba lake lililopo katika kitongoji cha Mputa mashambani Wilayani humo.

Aidha katika taarifa hiyo,Mashuhuda hao walieleza kuwa tukio hilo lilitokea majira ya jioni ya April 26 mwaka huu katika eneo la mashamba hayo baada ya marehemu kwenda kwa lengo la kuwafukuza baada ya kuwaona wakiwa wanashambulia maboga na mazao mengine shambani mwake.

Akizungumzia tukio hilo Mtendaji wa kijiji cha Luhangano Sidea Mbawala alisema kuwa katika tukio hilo marehemu akiwa na wenzake walikuwa wanawafukuza tembo hao ghafla tembo mwingine aliyekuwa na mtoto alitokea nyuma yao na kuanza kumshambulia.